Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Shambulio la kigaidi Burkina: Thelathini na sita wauawa katika Mkoa wa Sanmatenga

Burkina Faso inaendelea kukumbwa na zimwi la mauaji. Raia ndio wanaendelea kulengwa na mashambulizi hayo. Jumatatu wiki hii raia 36 waliuawa katika Mkoa wa Sanmatenga katika Jimbo la Kaskazini ya kati.

Mkoa wa Sanmatenga ambapo kinapatikana kijiji cha Yirgou kaskazini ya kati mwa Burkina Faso.
Mkoa wa Sanmatenga ambapo kinapatikana kijiji cha Yirgou kaskazini ya kati mwa Burkina Faso. fr.wikipedia.org
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa serikali, kundi la magaidi wenye silaha walivamia vijiji vya Nagraogo na Alamou na kuuwa watu 36. Serikali imetangaza siku mbili ya maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatano hii, Januari 22. Bendera zitapandishwa nusu mlingoti kwenye ofisi za serikali na balozi za nchi hiyo ugenini.

Jumatatu ni siku ya soko huko Nagraogo, kijiji kinachopatikana katika wilaya ya Barsalagho vijijini katika mkoa wa Sanmatenga. magaidi hao waliwashambulia raia wakiwa sokoni kwa kuwafyatulia risasi na kuuwa watu wengi.

Watu 32 waliuawa kwa mujibu wa serikali. Washambuliaji walichoma soko kabla ya kuondoka eneo la tukio.

Washambuliaji hao pia waliua watu wengine wanne katika kijiji cha Alamou, katika mkoa huo wa Sanmatenga, wanakijiji watatu pia walijeruhiwa kulingana na ripoti rasmi.

Washambuliaji hao pia walichoma kwa moto karibu pikipiki 30 za wakaazi wa maeneo yaliyoshambuliwa. Kulingana na duru za kuaminika, raia wametoroka vijiji hivyo na kukimbilia katika kijiji cha Kaya, kilomita zaidi ya mia moja Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.