Pata taarifa kuu
CAR-URUSI-RSF-USALAMA

RSF yataka uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya waandishi 3 wa Urusi Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka, limewataka maafisa wa usalama wanaochunguza mauaji ya wanahabari watatu wa urusi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2018 kutoa ripoti kamili ya uchunguzi wao.

Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.
Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za mwanzo zilisema Waandishi hao wa habari nhini Urusi waliuawa na watu wasiojulikana.

Shirika la RSF linasema licha ya kuwepo ukimya wa karibu miaka miwili sasa, ipo haja ya kuhakikisha ushahidi uliotolewa katika uchunguzi wa mwanzo, na njia zote zinafwatwa.

Vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na vile vya kimataifa viliripoti uwepo wa kundi la Wagner katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika Kati tangu Moscow ilipokabidhi silaha ndogo ndogo kwa idara za usalama za nchi hiyo na kupeleka mamia ya wakufunzi wa kijeshi na raia wa kawaida kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.