Pata taarifa kuu
LIBYA-MAZUNGUMZO-AMANI-UJERUMANI

Viongozi wa dunia wanakutana Berlin kuisaidia Libya kupata amani

Viongozi wa dunia wanakutana jijini Berlin nchini Ubelgiji, kushinikiza pande zinazozana nchin Libya kufikia mwafaka wa kuacha vita na kutia saini mkataba wa amani, kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 2011.

Lango la kuingia katika eneo la mkutano jijini Berlin nchini Ujerumani kuhusu mazungumzo ya Libya  Januari 19 2020
Lango la kuingia katika eneo la mkutano jijini Berlin nchini Ujerumani kuhusu mazungumzo ya Libya Januari 19 2020 © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hili ni jaribi la pili la mazungumzo haya, baada ya lile la kwanza kufanyika jijini Moscow nchini Urusi siku kadhaa zilizopita, lakini mwafaka haukupatikana.

Kansela wa Ujwerumani Angela Merkel, na viongozi kutoka Urusi, Uturuki, Ufaransa ni miongoni mwa viongozi wa dunia wanaohudhuria mazungumzo ambayo pia yanaungwa mkonoa na Umoja wa Mataifa.

Lengo kubwa la viongozi hawa wa dunia kuhudhuria mazungumzo haya, ni kutumia ushawishi wa kijeshi, kifedha au silaha kuisaidia Libya kupata amani na kuacha vita.

Hata hivyo, viongozi kutoka mataifa jirani kama Morocco, Tunisia na Ugiriki wanashtumu waandaji wa mazungumzo hayo, wakisema hawakualikwa.

Viongozi wanaokinzana , kiongozi wa wapiganai wa upinzani Khalifa Haftar na kiongozi wa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj wanahudhuria mazungumzo haya na wanakutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana tangu mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.