Pata taarifa kuu
ANGOLA-ISABEL DOS SANTOS-SIASA-HAKI

Isabel dos Santos kuwania kiti cha urais Angola

Binti wa za rais wa zamani wa Angola, Isabel dos Santos, amesema anafikiri kuwania urais mwaka 2022. Isabel, kama wengi wa wanafamilia ya dos Santos, aliondoka Angola, akidai alikabiliwa na vitisho vya kuuliwa baada ya baba yake kuondoka madarakani.

Isabel dos Santos, mwanamke wa kwanza tajiri barani Afrika.
Isabel dos Santos, mwanamke wa kwanza tajiri barani Afrika. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Isabel dos Santos anayeaminiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika anachunguzwa kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha na kuzisababishia hasara kubwa kampuni za serikali ikiwa ni pamoja na kampuni kubwa ya mafuta ya taifa  ‘Sonangol‘.

Viongozi wa mashtaka walizuia mali zake anazomiliki na mume wake Sindika Dokolo, raia wa DRC.

Taarifa zaidi zinasema kuwa hisa zao katika kampuni kadhaa za Angola, pamoja na kampuni ya simu ya Unitel  na kampuni ya simenti ya Cimangola, pia zimeshikiliwa na mahakama.

Mapema mwezi huu Binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos alikanusha madai ya ufisadi baada ya mahakama mjini Luanda kuifunga akaunti yake ya benki. Isabel dos Santos alisema madai hayo dhidi yake yamechochewa kisiasa.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa kampuni ya matuta ya taifa Sonangol mnamo mwaka 2016 lakini alitolewa kwenye wadhfa huo mwaka uliofuata wa 2017, katika hatua ya kwanza iliyofanywa na rais wa Angola Joao Lourenco ya kuwaondoa jamaa za dos Santos kutoka kwenye nyadhifa mbalimbali.

Baba yake Jose Eduardo dos Santos aliitawala Angola kwa miaka 38 na utawala wake unahusishwa na kukithiri kwa ufisadi na ubaguzi  kwa madai kwamba aliyekuwa rais dos Santos aliwapendelea watu wa familia katika kuwapa vyeo serikalini hadi Rais Joao Lourenco alipochukua nafasi yake mnamo mwaka 2017.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa kampuni ya matuta ya taifa Sonangol mnamo mwaka 2016 lakini alitolewa kwenye wadhfa huo mwaka uliofuata wa 2017
Aliteuliwa kuwa mkuu wa kampuni ya matuta ya taifa Sonangol mnamo mwaka 2016 lakini alitolewa kwenye wadhfa huo mwaka uliofuata wa 2017 REUTERS/Siphiwe Sibeko
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.