Sudan, Ethiopia, Misri, wafikia makubaliano ya matumizi ya Mto Nile
Jitihada zinaendelea kupigwa kati ya Ethiopia, Misri na Sudan katika mazungumzo ya matumizi ya maji ya Mto Nile. Nchi hizo tatau zimekubaliana kutumia maji ya Mto huyo Nile
Imechapishwa:
Mazungumzo hayo yanayongozwa na Marekani, na pande zote zilikuwa zimekubaliana kuwa kufika jana mwafaka uwe umepatikana, lakini Mawazier wa Mambo ya nje wa mataifa hayo matatu sasa wasema kufikia tarehe 28 au 29 mwezi huu mkataba utakuwa umefikiwa.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi tatu, pamoja na Marekani na Benki ya Dunia, imesema kwamba washiriki wanaojadiliana wamekubaliana kujaza bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia wakati wa msimu mvua kati ya miezi ya Julai na Agosti.
Hata hivyo taarifa hiyo haikusema lolote kuhusu masuala ya msingi yanayozunguka mgogoro huo ambayo ni kasi ya kujaza bwawa hilo
Ethiopia inatumia maji ya Mto Nile kujenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme, huku Misri ikilalamika kuwa, hatua hiyo itasaiabibisha wananchi wake kukosa maji kwa sababu mto huo ndio chanzo pekee cha maji.
Makubaliano ya mwisho yatatiwa saini Januari 28-29, wakati ambapo mawaziri kutoka nchi tatu watakuwa wanakutana Washington.