COTE D'IVOIRE-USALAMA
Watoto 137 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Magharibi waokolewa
Serikali ya Cote d'Ivoire imeokoa watoto 137 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Magharibi ambao wamekuwa wakifanyishwa kazi kama vubarua na wengine kujihusisha na biashara hatari ya kuuza miili yao.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hii imekuja, baada ya operesheni maalum kufanyika katika jimbo la Aboisso, karibu na nchi ya Ghana.
Watoto hao waliokolewa wanatokea nchini Nigeria, Niger,Benin, Ghana na Togo.
Watu 12 wanaoshukiwa kuhusika na biashara haramu ya kuwasafirisha watoto hao nchini humo, wamekamatwa.