Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA-USALAMA

Yahya Jammeh aweka wazi nia yake ya kurudi Gambia

Rais wa Zamani wa Gambia, Yahya Jammeh, aliyelazimika kuachia madaraka na kukimbilia uhamishoni, amevunja ukimya wake, na kubaini kwamba yuko tayari kurejea nchini Gambia.

Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017
Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017 © REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Yahya Jammeh, ambaye alitawala kwa mkono wa chuma kwa miaka 22 na ambaye anaendelea kuishi uhamishoni kwa miaka mitatu nchini sasa, nchini Equatorial Guinea, alisikika mwishoni mwa wiki hii iliyopia nchini Gambia kupitia sauti iliyorekodiwa. Katika sauti yake iliyorekodiwa kwa simu, Yahya Jammeh amebaini kwamba anatamani kurudi nchini mwake.

Sauti hiyo ilisikika kupitia mitandao ya kijamii. Yahya Jammeh alikuwa akizungumza kwa njia ya simu na afisa wa chama chake. Katika mazungumzo hayo, Yhaya Jammeh ametoa ushauri wa jinsi ya kufanya maandamano yaliyopangwa na chama chake cha siasa, Alhamisi wiki jijini Banjul.

Kufikia sasa, hakuna jipya ambalo limekwisha fanyika, kwani sauti zake nyingi zilizorekodiwa, ambazo zilivuja, zilisikika akitoa ushauri kwa chama chake cha siasa.

Lakini jipya katika mazungumzo hayo ya sasa, Yahya Jammeh ameelezea kwa mara ya kwanza, kwa njia iliyo wazi kabisa, nia yake ya kurudi nchini Gambia. Amewahimiza wafuasi wake kuelezea nia yake kwa mamlaka nchini Gambia, ambayo amesema inapaswa kutekeleza hayo kwa mkataba, akimaanisha ahadi iliyotolewa na Umoja wa Afrika, ECOWAS na Umoja wa Mataifa, wakati alipokubali kuondoka madarakani, kwa kuheshimu haki zake, na haswa ile ya kurudi nyumbani siku moja, kama raia na rais wa zamani wa nchi hiyo.

Tangazo hili linakuja wakati muungano wa vyama uliompatishia ushindi Adamu Barrow kukumbwa na mgawanyiko mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.