Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Niger: Serikali yathibitisha vifo vya askari 89 Chinagoder

Baraza la usalama la kitaifa nchini Niger limeweka wazi taarifa kuhusu vifo vya askari wake waliouawa katika mapigano katika kambi ya Chinagoder. Serikali imethibitisha idadi ya askari 89 waliouawa katika mapigano hayo.

Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria (picha ya kumbukumbu). ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanaigeria wengi hawakuelewa ukimya huu wa serikali kuhusu idadi ya askari waliuawa katika mapigano hayo.

Siku nne baada ya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Chinagoder, magharibi mwa Niger, karibu na mpaka wa Mali, Baraza la usalama la kitaifa limetoa heshima za mwisho kwa askari 89 rasmi waliuawa katika mapigano hayo katika taarifa iliyosomwa na msemaji wa serikali, Zakaria Abdourahame, kwenye redio ya umma.

Baraza la usalama la kitaifa limeapa kuendelea na mapambano dhidi ya ugaidi hadi ushindi wa mwisho, amesema Bw Abdourahame.

Wanajihadi sabini na saba waliangamizwa huko Chinagoder, kwa mujibu wa Zakaria Abdourahame.

Vikosi vya jeshi la Niger vimemshinda adui na kumtimuwa hadi nje ya mipaka ya Niger, ameongeza msemaji wa serikali ya Niger.

Wakati huo huo, siku tatu ya maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kuanzia Jumatatu hii, Januari 13. Bendera zitapeperushwa nusu mlingoti nchi nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.