Pata taarifa kuu
CAR-DJOTODIA-SIASA-USALAMA

Rais wa zamani Michel Djotodia arejea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia, aliyekuwa akiishi uhamishoni Benin tangu mwaka 2014, amewasili leo Ijumaa, asubuhi Januari 10, 2020 jijini Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia, aliporudi Bangui, Januari 10, 2020.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia, aliporudi Bangui, Januari 10, 2020. © FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Michel Djotodia, kiongozi wa zamani wa kundi la zamani la waasi la Seleka, alichukuwa madaraka mnamo mwaka 2013 baada ya kumpindua madarakani François Bozize.

Miaka sita baada ya kuondoka Bangui, Bw Djotodia amewasili jijini Bangui kwa ziara ya siku mbili.

Rais huyo wa zamani alikutana na familia yake mara tu alipowasili kabla ya kuelezea sababu za kurudi kwake.

"Nimekuja kutoa salamu zangu za Mwaka Mpya, na kupendekeza kuwa ninaweza kuchangia kwa ujenzi wa nchi. Nitakutana narais, nitamsikiliza, halafu tutaangalia jinsi ya kuweka mambo sawa. Sintokutana kwa mazungumzo na watu kwa sasa, mkutano wa wakuu wa zamani wa nchi, mawaziri wakuu wa zamani na viongozi wa vyama vya siasa, nadhani kuwa siku zijazo nitatakiwa kurejea nchini, " amesema Michel Djotodia.

"Mimi si mtu wa vita tena, sasa niko mtu wa amani. Kwa hivyo nitawatoa hofu baadhi ya watu wenye mawazo kama hayo. Badala yake, nimekuja kusaidia wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. inabidi raia hawa waishi kwa amani. Wamechoshwa na vita. Na hatutaruhusu mtu yeyote kuchukua silaha na kuwahangaisha akina mama, watoto na wazee nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hatutaruhusu na hakuna tena waasi ambao wako msituni, " ameongeza Bw Djotodia.

Michel Djotodia atakutana na Rais Touadéra na wadau wote. Kuwasili kwake Bangui kunakuja wiki tatu tu baada ya rais mwingine wa zamani François Bozizé kurejea nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.