Pata taarifa kuu
DRC-ELIMU-USALAMA

DRC: Mamlaka yafunga Chuo Kikuu cha Kinshasa kufuatia machafuko

Mamlaka nchini DRC imeamua kufunga Chuo Kikuu cha Kinshasa, UniKin, kwa sababu ya ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea chuoni hapo kwa siku mbili.

Chuo Kikuu cha Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Chuo Kikuu cha Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (CC)/Humprey J. L. Boyelo/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuongezwa ada ya chuo kikuu kwa wanafunzi wanaolipa kwa sarafu ya Faranga za Congo imezidisha mtafaruku mkubwa kwenye chuo kikuu hicho. Afisa wa polisi ameuawa kwa kupigwa mawe katika makabiliano kati ya wanafunzi na vikosi vya usalama.

Licha ya wito wa utulivu uliotolewa Jumatatu jioni na Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga, ghasia zilianza tena Jumanne kati ya wanafunzi na polisi katika chuo kikuu cha Kinshasa.

Serikali imeamua kusimamisha shughuli zote katika chuo kikuu hicho.

Waziri wa Elimu ya Juu Thomas Luhaka ameomba vikosi vya usalama "kubaini na kuwakamata haraka iwezekanavyo wanaosababisha uhalifu huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.