Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Libya: Vikosi vya Khalifa Haftar vyadhibiti mji wa Sirte

Baada ya kulenga mji mkuu wa Libya, Tripoli, tangu mwezi Aprili 2019, vikosi vya Marshal Khalifa Haftar vinadhibiti mji wa Sirte tangu jana Jumatatu Januari 6, 2020.

Ahmad al-Mesmari, msemaji wa vikosi vya Khalifa Haftar, akizungumza na wanahabari, katika mji wa mashariki wa Benghazi, ametangaza kwamba mji Sirte, uandhibitiwa na vikosi vyao tangu Januari 6, 2020.
Ahmad al-Mesmari, msemaji wa vikosi vya Khalifa Haftar, akizungumza na wanahabari, katika mji wa mashariki wa Benghazi, ametangaza kwamba mji Sirte, uandhibitiwa na vikosi vyao tangu Januari 6, 2020. © Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mji huo wa Sirte ulioko katikati mwa Libya, kwenye umbali wa kilomita 250 kutoka Misrata, ngome ya wanamgambo wanaounga mkono Serikali ya umoja wa kitaifa, umedhibitiwa kutoka mikonini vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Operesheni hiyo ilidumu saa chache tu.

Kwa mujibu wa afisa wa vikosi vya Khalifa HAftar, mji wa Sirte uko mikononi mwa vikosi vya ANL tangu Jumatatu jioni. Askari huyo, ambaye alizungumza kwenye televisheni kadhaa za Libya na Misri, anadai kwamba mji wa pwani ulianguka mikononi mwa vikosi vya Khalifa Haftar kwa muda wa saa chache, vikosi vya jeshi ambavyo vilikuwa vinaushikilia, vilitimka mapema.

Majeshi hayo ANL ambayo yalisaidiwa na ndege katika vita hivyo, yanadai kwamba yameshambulia mji huo kutoka sehemu tano. Vikosi maalum vya Mashariki viliteka kwanza uwanja wa ndege wa kijeshi na uwanja wa ndege wa Kardabaya.

Hayo yanajiri wakati rais wa Recep Tayyip Erdogan alitangaza hivi karibuni kwamba Ururuki iko tayari kuwatuma askari wake nchini Libya kusaidi majeshi ya serikali ya umoja wa kitaiafa, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.