Pata taarifa kuu
CHAD-UCHUMI-USALAMA

Chad: Sekta ya umma kukumbwa na mgomo kufuatia kukwama kwa mazungumzo

Kuanzia Jumanne hii sekta ya umma nchini Chad itakumbwa na mgomo. Watumishi wa umma wanaanza mgomo wakidai kuwa wanasubiri kulipwa marupurupu yao na posho vilivyokatwa kwa miaka mitatu.

Moja ya kata za Ndjamena kushuhudia mgomgo wa watumishi wa umma.
Moja ya kata za Ndjamena kushuhudia mgomgo wa watumishi wa umma. © MASBEYE BOYBEYE RENAUD/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wameamua kufanya mgomo baada ya mazungumzo kati yao na serikali kutozaa matunda yoyote.

Baada ya mazungumzo yaliyofanyika Jumatatu hii, Januari 6, wakati serikali ilijaribu kushawishi kutofanya mgomgo huo, wafanyakazi wameapa kuwa wako tayari kuanza mgomo Jumanne hii asubuhi, huku wakitarajia kubadilisha mbinu kila baada ya siku tatu.

"Ikiwa tutafanya mgomo kwa siku tatu wiki hii, tunapaswa kufikiria njia nyingine ya kutumia. Je mgomo huu unapaswa kuambatana na maandamano mbele ya ofisi zetu? ... tunatakiwa kufanya hivyo kila baada ya siku tatu ili kuhofia kufanya yote hayo kwa mara moja, "amebaini Barka Michel, msemaji wa muungano wa vyama vya wafanyakazi.

Serikali - ambayo imeshtumu mgomo huo kwamba haukufuata sheria - imelaani hatua ya vyama vya wafanyakazi ambavyo vimeamua kusitisha kazi wakati mazungumzo yanaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.