Pata taarifa kuu
CHAD-SENEGAL-HAKI

Hissene Habre mfungwa wa jamii ya kimataifa

Katika barua kwa viongozi wa Senegal, Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso inapinga kuachiliwa huru kwa Hissène Habré, rais wa zamani wa Chad.

Julai 20, siku ya kwanza ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Chad Hissène Habre alifukuzwa kwa nguvu kutoka mahakamani.
Julai 20, siku ya kwanza ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Chad Hissène Habre alifukuzwa kwa nguvu kutoka mahakamani. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Hissène Habré alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa makosa ya mateso, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Afisa wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch Reed Brody akihojiwa na RFI, amebaini kwamba kuachiliwa huru kwa Hissène Habré, "muuaji, ambaye aliwafanyiwa mateso watu wengi" miaka minne baada ya kuhukumiwa, ni kinyume na sheria ya msingi ya Senegal.

"Hii inamaanisha kwamba mkataba dhidi ya mateso unazitaka nchi kukabiliana na vitendo vya mateso kwa njia ya adhabu ambayo inazingatia uzito wa vitendo hivi", Reed Brody amesema.

"Kwa hivyo mtu ambaye amehukumiwa miaka nane kwa makosa ya kuwatesa raia hawezi kusamehewa chini ya miaka minne baada ya kupatikana na hatia", ameongeza afisa huyo wa shirika la kimataifa la haki za binadamuu la Human Riht Watch.

Reed Brody akimnukuu Waziri wa Sheria wa Senegal Malick Sall, Hissène Habré sio mfungwa wa Senegal, ni mfungwa wa jamii ya kimataifa.

Awali serikali ya Ubelgiji iliitaka serikali ya Senegal imfungulie mashtaka Habre au imkabidhi kwa ajili ya kuhukumiwa nchini Ubelgiji. Baada ya Senegal kukataa ombi hilo Ubelgiji imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kuchukua hatua.

Hissène Habré anakabiliwa na tuhuma za kuua maelfu ya watu na kutesa wengine wengi katika kipindi cha utawala wake wa kati ya mwaka 1982 hadi 1990 nchini Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.