Pata taarifa kuu
AFRIKA-MWAKA MPYA-SIASA-USALAMA-UCHUMI

Viongozi wengi wa Afrika watoa salaamu za Mwaka Mpya kwa raia wao

Jumanne jioni Desemba 31, wakuu wengi wa nchi za Kiafrika walipeleka salaamu za mwaka mpya kwa raia wa mataifa yao, wakiweka bayana kile walichotekeleza mwaka uliopita na matarajio ya mwaka 2020.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, IBK, alitoa heshima kwa askari wote waliokufa katika vita dhidi ya ugaidi mwaka 2019.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, IBK, alitoa heshima kwa askari wote waliokufa katika vita dhidi ya ugaidi mwaka 2019. Issouf Sanogo/AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, IBK, alitoa heshima kwa askari wote waliokufa katika vita dhidi ya ugaidi mwaka 2019, mapigano ambayo pia rais wa Tchad Idriss Déby Itno aligusia, huku akilaumu jumuiya kimataifa kwa kutofanya lolote.

Nchini Gabon, hotuba ya rais Ali bongo Ondimba iligubikwa hasa na vita dhidi ya ufisadi. Karibu mwezi mmoja baada ya kukamatwa kwa mkuu wake wa zamani wa ofisi ya rais, Ali Bongo amesema "wale wote wataojihusisha na vitendo vya ufisadi wataadhibiwa bila ubaguzi"

Naye rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Dramane Ouattara, amesifu rekodi yake ya kijamii kwa kuashiria kupungua kwa umasikini. Pia amegusia kuhusu tuhuma dhidi ya mpinzani wake Guillaume Soro: "Hakuna jaribio lolote la kuyumbisha usalama linaweza kufanikiwa”, huku akiahidi kuandaa uchaguzi wa amani mwaka huu wa 2020.

Huko Guinea, rais Alpha Condé amegusia maandamano ya vurugu ambayo yameshuhudiwa mwisho wa mwaka wa 2019. huku akirejelea tena kwenye mpango wake wa kurekebisha Katiba akitangaza kwamba anataka kuiwasilisha kwa wananchi kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi.

Na nchini DRC, 2020 itakuwa mwaka wa hatua kwa Félix Tshisekedi. Katika hotuba yake, Tshisekedi Tshilombo amesema anataka kuanzisha mfumo mpya wa utawala ili kukidhi vipaumbele vya nchi.

Upande wake rais wa Rwanda Paul Kagame, amewataka wananchi wake kutobweteka na mafaaniko wanayopata, na hivyo amewatolea wito kujibidisha zaidi katika sekta mbalimbali.

Nchini Uganda rais Museveni amewataka wananchi kuipenda nchi yao na bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.