79 wauawa katika shambulizi mjini Mogadishu
Idadi ya vifo vilivyotokana na Mlipuko mkubwa wa bomu lililokuwa limetegwa katika eneo lenye shughuli nyingi mjini Mogadishu nchini Somalia imeongezeka na kufikia 79 na majeruhi kadhaa,likiwa ni shambulizi jingine baya ndani ya miaka miwili nchini humo.
Imechapishwa:
16 kati ya waliofariki walikuwa wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Binafsi Banadir kilichopo mjini Mogadishu waliokuwa safarini mara mlipuko ulipotokea kusini magharibi mwa jiji hilo.
Majeruhi wengi walibebwa kwa machela na kuondolewa katika eneo la mkasa ambapo mlipuko ulivuruga na kusalia mabaki ya magari.
Raia 2 wa Uturuki ni miongoni mwa waliouawa,kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Uturuki ambayo iliarifu kupitia ukurasa wake wa Twita.
Bado haijajulikana nani hasa wahusika wa shambulizi hilo licha ya mashambulizi kadhaa kutekelezwa na kundi la kiislamu Al shabab ambalo limekuwa likipambana na serikali inayoungwa mkono na umoja wa mataifa.