Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Islamic State yaua mateka wa Kikristo nchini Nigeria

Kundi la Islamic State limetoa video inayoonyesha mauaji ya Wakristo 11 nchini Nigeria. Kundi la Islamic State limebaini kwamba ni sehemu ya kampeni yake iliyotangazwa hivi karibuni ya 'kulipiza kisasi' kifo cha kiongozi wake na msemaji wake aliyeuawa nchini Syria mnamo mwezi Oktoba.

Askari wa jeshi la Nigeria wakipiga doria katika mji wa Maiduguri, katika Jimbo la Borno, Nigeria, Agosti 31, 2016.
Askari wa jeshi la Nigeria wakipiga doria katika mji wa Maiduguri, katika Jimbo la Borno, Nigeria, Agosti 31, 2016. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Hakuna maelezo ambayo yametolewa kwa waathiriwa, ambao wote walikuwa wanaume, lakini IS inasema 'walitekwa wiki zilizopita' katika jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Borno.

Video hiyo ya sekunde 56 ilitengenezwa na 'shirika la habari' la Islamic State Amaq.

Video hiyo ilirushwa hewani Desemba 26 na wachambuzi wanasema ilikuwa inaambatana na sherehe za Krismasi.

Picha hizo zilipicha katika eneo lisilojulikana. Mmoja wa wafungwa aliyekuwa katikati aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wengine 10 wawalichinjwa.

Abu Bakr al-Baghdadi na Abul-Hasan Al-Muhajir, afisa wa zamani wa kundi la Islamic State, waliuawa nchini Syria mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Miezi miwili baadaye, Desemba 22, kundi la Islamic State lilitangaza kampeni mpya ya 'kulipiza kisasi' kifo chao na tangu wakati kuni hilo lilidai kuhusika na mashambulizi mengi katika nchi mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.