Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Watu 11 wauawa katika makabiliano Bangui

Makabiliano kati ya wanamgambo na wafanyabiashara yaliyozuka Jumatano jioni na kuendelea leo Alhamisi katika eneo lenye Waislamu wengi la PK5 jijini Bangui, yameua watu wasiopungua kumi na moja, kwa mujibu wa Imamu mkuu wa eneo hilo na vyanzo viwili vya usalama.

Wakazi wa eneo lenye Waisilamu wengi la PK5 wakipandwa na hasiri baada ya kushambuliwa. Aprili 10, 2018.
Wakazi wa eneo lenye Waisilamu wengi la PK5 wakipandwa na hasiri baada ya kushambuliwa. Aprili 10, 2018. FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

'Miili 16 ililetwa msikitini,' Awad Al Karim, imamu wa msikiti wa Ali Babolo, katika eneo la PK5 ameliambia shirika la habari la AFP. PK5 ni eneo ambalo limeshindwa kudhibitiwa na viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na vikosi vya Umoja wa Matiafa, vyanzo viwili vya usalama vimebaini.

Mpaka leo Alhamisi idadi rasmi ya waliouawa katika makabiliano hayo ilikuwa bado haijajulikana.

'Makabiliano yanaendelea, na tumetuma kikosi maalumu kwa lengo la kuzima ghasia hizo. Sehemu moja ya soko imeteketezwa kwa moto, pamoja na magari kadhaa,' amesema Bili Aminou Alao, msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA.

'Kati ya maduka 40 hadi 50 yamechomwa moto, pamoja na nyumba nne hadi tano," Kanali Patrick Bidilou Niabode, mkurugenzi mkuu wa kikosi cha Zima Moto nchini jamhuri ya Afrika ya Kati, ameliambia shirika la habari la AFP.

Licha ya kupungua kwa ghasia tangu kusainiwa kwa mkataba wa amani Februari 6 kati ya serikali ya Bangui na makundi 14 yenye jeshi, nchi hiyo bado inakabiliwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya wanamgambo waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.