Pata taarifa kuu
SUDAN-ICC-BASHIR-SIASA

Rais wa zamani wa Sudan aanza kuchunguzwa kuhusu mauaji ya Darfur

Nchi ya Sudan imefungua rasmi uchunguzi kuhusu makosa ya kivita yaliyotekelezwa kwenye jimbo la Darfur na rais wa zamani wa taifa hilo Omar al-Bashir pamoja na washirika wake wengine zaidi ya 50.

Rais wa Sudan Omar al Bashir
Rais wa Sudan Omar al Bashir REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali Tagelsir al- Heber, amesema ofisi yake tayari imeanza kuchunguza makosa yaliyotekelezwa Darfur kuanzia mwaka 2003, huku akiwataja viongozi wa zamani zaidi ya 50 akiwemo al-Bashir kuwa ni miongoni mwa wanaochunguzwa.

Uchunguzi huu utakuwa ni wa kwanza kuanzishwa tangu al-Bashir aondolewe madarakani na jeshi mwezi April baada ya maandamano ya kupinga utawala wake uliodumu kwa miaka 30.

Bashir ambaye kwa sasa yuko kizuizini kwa makosa ya rushwa huku akisubiri kesi nyingine zinazomkabili, anatakiwa pia na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ambayo kupitia mwendesha mashtaka wake mkuu Fatou Bensouda imesema inatoa muda zaidi kwa Sudan kufanya uchunguzi wake.

Machafuko kwenye jimbo la Darfur yalianza mwaka 2003 baada ya waasi kutoka jamii ndogo iliyodai walikuwa wakitenga, kuchukua silaha na kuanza kupigana na Serikali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.