Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-MAASKOFU-KATOLIKI-UCHAGUZI 2020

Nkurunziza kuondoka madarakani 2020

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa mara nyingine amebainisha msimamo wake wa kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Hatua ambayo imeonekana kuwashangaza raia wengi wa Burundi huku wapinzani wake wakijiuliza ikiwa kauli yake itakuwa na ukweli.

Le président burundais Pierre Nkurunziza le 7 juin 2018.
Le président burundais Pierre Nkurunziza le 7 juin 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Rais Nkurunziza ameyasema hayo mwishoni mwa juma mbele ya maafisa wa jeshi na polisi kwenye sherehe zilizokuwa zimeandaliwa na taasisi hizo kumtakia siku kuu njema za mwisho wa mwaka.

Hatua hii inakuja wakati huu kukiwa na uvumi kwamba kiongozi huyo wa taifa la Burundi ana nia ya kuwania kiti cha uraisi katika uchaguzi ujao.

Burundi inaingia mwaka 2020 ikiwa na kumbukumbu ya visa vya mauaji na mivutano ya kisiasa vilivyoshuhudiwa mwaka 2019 ikiwa imesalia miezi kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais nchini humo.

Visa vya kuteketezwa kwa moto ofisi ndogo za chama kikuu cha upinzani cha CNL, katika maeneo mbalimbali ya nchi vilishuhudiwa, huku chama hicho kikinyooshea kidole cha lawama vijana kutoka chama tawala, CNDD-FDD, Imbonerakure kuhusika na visa hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.