Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Rais Alpha Conde atangaza rasimu ya katiba mpya

Rais wa Guinea Alpha Conde amesema ataanzisha mjadala wa kitaifa ili katiba ya nchi hiyo ifanyiwe marekebisho kupitia kura ya maoni. Katika hotuba yake, Rais huyo wa Guinea amesema kuwa tume ya ufundi tayari imeshafanya kazi chini ya uongozi wa Waziri wa Sheria, ambaye ametunga rasimu ya Katiba.

Rais wa Guinea, Alpha Conde.
Rais wa Guinea, Alpha Conde. ©FREDERICK FLORIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kwa muda mrefu, mjadala kuhusu haja ya kuitafutia Jamhuri ya Guinea Katiba mpya ili kuchukua nafasi ya ile ya Mei 7, 2010 imeanza katika nchi yetu," amesema Alpha Condé. Kwa kuzingatia kigezo cha msingi na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na kiongozi wa serikali, ninaagiza Waziri wa Sheria, anayesimamia uhusiano na taasisi za jamhuri, kuchukua hatua za kuandaa rasimu ya Katiba katika maana ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau wote walioshiriki katika mazungumzo. "

Hatua hii inatathminiwa na wapinzani wake kuwa, ni mbinu ya Cinde mwenye umri w amiaka 81, kutaka kuendelea kuwa madarakani, baada ya muhula wake kumalizika mwaka ujao.

Tangu mwezi Oktoba, kumekuwa na maandamano ya kupinga mchakato wowote wa kuibadilisha katiba na kumruhusu rais huyo aliyeingia madarakani mwaka 2010 kuwania tena urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.