Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA-LAMUKA

Katumbi atangaza kuunda chama chake, aachana na Lamuka

Wafuasi wa Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga na mbunge wa upinzani Moise Katumbi Chapwe wamekuwa wakikutana mjini Lubumbashi nchini DRC, kuunda chama kipya, baada ya mwanasiasa huyo kujiondoa kwenye muungano wa Lamuka, unaoongozwa na aliyekuwa mgombea urais Martin Fayulu.

Moïse Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC
Moïse Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Junior KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katumbi amesema lengo lake ni kuimarisha hali ya kisiasa na kuendelea kupigania demokrasia ncgini humo pamoja na uongozi bora katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

“Kila mahali watu wanakosa uvumilvu. Ni sharti tuugane ili kuunda chama kitakachopigania mabadiliko na kushughulikia wananchi,” alisema.

Vyama vya Ensemble pour le changement kimesema kuwa kinaungana na Katumbi, katika harakati hizi mpya, baada ya kukutana wiki hii jijini Lubumbashi.

Wachambuzi wa siasa wanahoji hatima ya wabunge ambao wamejiunga na Katumbi, baada ya kuondoka kwenye vyama vyao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.