Pata taarifa kuu
RSF-WAANDISHI WA HABARI-HAKI-USALAMA

Ripoti ya RSF: Waandishi wa habari 49 ulimwenguni kote waliuawa mwaka 2019, 389 walifungwa

Shirika la kimataifa linalotetea haki ya waandishi wa habari, RSF, limetoa ripoti ambamo linabaini kwamba waandishi wa habari 49 wameuawa mwaka huu na 389 wamefungwa jela.

Nembo ya shirika la kimataifa linalotetea haki ya waandishi wa habari (RSF).
Nembo ya shirika la kimataifa linalotetea haki ya waandishi wa habari (RSF). ©rsf
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya waandishi wa habari waliouawa imepungua asilimia 50 mwaka huu. Kiwango hiki ambacho ni cha 'chini kihistoria' kinahusishwa katika maeneo ya mizozo iliyosababisha idadi ndogo ya vifo kuliko mwaka 2018, kwa mujibu wa Ripoti ya shirika linalotetea haki ya waandishi wa habari RSF.

Waandishi wa habari arobaini na sita wa kiume na wanawake watatu waliuawa mwaka wa 2019 duniani kote. Mwaka 2018 waandishi wa habari themanini waliuawa. Kati yao, 29 waliuawa katika maeneo yenye amani na zaidi ya 60% walilengwa.

Hakuna mwandishi wa habari aliyeuawa wakati akiwafanya kazi yake nje ya nchi, wote waliouawa walikuwa wakifanya kazi katika nchi zao.

Kwa upande mwengine idadi ya waandishi wa habari waliofungwa, iliongezeka hadi 12%.

Idadi ya waandishi wa habari 389 waliofungwa mwaka 2019 inatia 'wasiwasi zaidi kwani kwenye idadi hiyo haijumuishwi idadi ya waandishi wa habari waliokamatwa kiholela au kuzuiliwa kwa masaa kadhaa, kwa siku kadhaa au hata kwa wiki kadhaa', imebaini RSF, ambayo imeongeza kuwamba idadi ya waandishi walio kamatwa iliongezeka mwaka uliopita, kwa sababu ya maandamano na matukio mengine yaliyotokana na maandamano kote ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.