Pata taarifa kuu
UFARANSA-COTE D'IVOIRE-USHIRIKIANO

Macron na Ouattara kutoa heshima zao kwa wahanga wa Bouaké

Miaka kumi na tano baada ya shambulio la anga Bouaké, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, Jumapili, Desemba 22, watatoa heshima zao kwa askari tisa wa Ufaransa na askari mmoja wa Marekani waliouawa Novemba 6, 2004.

Alassane Ouattara na Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Elysée Juni 11, 2017.
Alassane Ouattara na Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Elysée Juni 11, 2017. © REUTERS/Mal Langsdon
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo ni la kwanza kufanyika, na kuhudhuriwa na marais kutoka nchi hizi mbili.

Marais wa Ufaransa na Côte d'Ivoire wataenda kwenye shule ya upili ya Descartes, ambapo kulikuwa kambi ya Ufaransa iliyolengwa na shambulio la jeshi la Côte d'Ivoire wakati wa utawala wa Laurent Gbagbo dhidi ya waasi.

Shambulio hilo lilisababisha mvutano mkali kati ya Ufaransa na Côte d'Ivoire. Chanzo cha shambulio hilo mpaka sasa hakijaelezwa.

Emmanuel Macron na Alassane Ouattara watakuwa pamoja katika eneo lililoshambuliwa la Bouaké. Hii ni moja ya matukio makubwa ya ziara ya rais wa Ufaransa nchini Côte d'Ivoire.

Emmanuel Macron atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kuzuru eneo hilo tangu shambulio lilipotokea. Shule ya upili ya Descartes, ambapo kulikuwa kambi ya jeshi la Ufaransa tangu wakati huo ilikarabatiwa na kuwa kama jengo la serikali, lakini athari za mabomu yaliyorushwa dhidi ya kambi hiyo mwaka 2004 zinaonekana hadi leo.

Rais wa Ufaransa ataweka shada za maua na jiwe la msingi la ujenzi wa mnara kwenye makaburi ya askari waliouawa. Hii ni 'ishara muhimu katika uhusiano wa Ufaransa na Côte d'Ivoire', Élysée imebaini katika taarifa. Mashambulizi haya yalikwamisha kwa miaka mingi uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kusababisha kurudisha maelfu ya raia wa Ufaransa kurejeshwa nyumbani.

Rais wa Ufaransa atazuru Côte d'Ivoire kuanzia Desemba 20 hadi 22 kwa kusherehekea sikuu kuu za Mwisho wa mwaka akiambatana na kikosi cha askari wa Ufaransa wanaopiga kambi nchini Mali.

Rais Emmanuel Macron atakula chakula cha jioni cha Krismasi na askari wa Ufaransa katika kambi ya Port-Bouët, karibu na mji wa Abidjan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.