Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Waathiriwa wa mauaji ya Yumbi waendelea kusubiri kutendewa haki

Ni Mwaka mmoja leo, tangu kutokea mauaji ya mamia ya raia wa DRC katika eneo la Yumbi, katika mkoa wa Mai-Ndombe, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), katika usiku wa kuamkia uchaguzi mkuu.

Makao makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) huko Yumbi miongoni mea majengo yaliyochomwa.
Makao makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) huko Yumbi miongoni mea majengo yaliyochomwa. © RFI / Patient Ligodi
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Desemba 16, 17 na 18, 2018, Kwa mujibu wa Umoja aw Mataifa, shambulio la kikatili lililopangwa liligharimu maisha ya watu wasiopungua 535 na 111 kujeruhiwa katika eneo la Yumbi, lakini pia Bongende na Nkolo II, katika mkoa wa Mai-Ndombe, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Wakaazi wa maeneo hayo ambao wengi waliayahama makaazi yao baada ya mshambulio hilo na kukimbilia katika maeneo salama hasa katika mji wa Kinshasa wamekataa kurudi katika makaazi yao, wakisema bado wanakumbuka mengi kuhusu mauaji hayo.

Watu 20,000 waliyahama makaazi yao na 16,000 walikimbilia nchi jirani ya Congo-Brazzaville, ambapo anaishi katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.