Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAHEL-NIGER-USALAMA

Sahel: Ufaransa yaahirisha mkutano wa kilele wa Pau kufuatia shambulio Inates, Niger

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtaka mwenzake wa Nigeria Mahamadou Issoufou kukubaliana juu ya kuahirishwa kwa mkutano huo wa kilele (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtaka mwenzake wa Nigeria Mahamadou Issoufou kukubaliana juu ya kuahirishwa kwa mkutano huo wa kilele (picha ya kumbukumbu). © Ludovic MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Élysée imetangaza kwamba kwa sababu ya shambulio la wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali nchini Niger Jumanne wiki hii, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwa makubaliano na mwenzake wa Niger Mahamadou Issoufou, ameamua kuahirisha hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 mkutano na viongozi wa nchi tano za Sahel uliyopangwa kufanyika nchini Ufaransa Desemba 16.

Jumatano jioni Rais Emmanuel Macron alimwita Rais wa Nigeria Mahamadou Issoufou na wote wawili walikubaliana "kupendekeza wenzao kuahirisha hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 mkutano kuhusu kikosi cha Ufaransa cha Barkhane na kikosi cha pamoja cha nchi tano G5 Sahel uliopangwa kufanyika nchini Ufaransa, " ikulu Élysée imebaini, na kuongeza kwamba rais wa Ufaransa ameonyesha" uungwaji wake mkono na mshikamano wake "kwa mwenzake wa Niger kufuatia shambulio dhidi ya kambi la jeshi ya Inates.

Wakati huo huo Ufaransa imetuma mkuu wa majeshi ambaye atakutana kwa mazungumzo na Rais Issoufou. Ikulu ya Élysée inasema kwamba marais hao wawili wameonyesha nia yao ya kuendelea kuwa na mshikamano dhidi ya vitisho vya makundi ya kigaidi na 'kufafanuwa pamoja mfumo wa kisiasa na kiutendaji kwa kuchukua hatua kwa usalama wa raia na nchi za Sahel'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.