Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Libya yaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe

Libya inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miezi nane sasa. Vita hivyo vinahusisha kambi mbili hasimu nchini humo. Vita hivyo vimesababisha watu engi kupoteza maisha na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Hifadhi ya mafuta ya al-Sharara nchini Libya, kilomita 900 kusini mwa Tripoli.
Hifadhi ya mafuta ya al-Sharara nchini Libya, kilomita 900 kusini mwa Tripoli. © REUTERS/Ismail Zitoun
Matangazo ya kibiashara

Vita kati ya jeshi la mbabe wa kivita kutoka Mashariki mwa Libya Marshal Khalifa Haftar na jeshi linalounga mkono serikali ya Tripoli inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa imeendelea kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo lengo ni kudhibiti maeneo yenye visima vya mafuta.

Kila upand unajaribu kuonyesha nguvu zake kabla ya mkutano wa kimataifa jijini Berlin, nchini Ujerumani.

Jumatano alfajiri wiki hii, askari wengi wakiwa katika magari ya kijeshi walivamia eneo la visima vya mafuta la al-Fil, hifadhi kubwa ya mafuta nchini, eneo linalopatikana jangwani kusini magharibi mwa nchi.

Jeshi la ANL linaloongozwa na Marshal Khalifa Haftar, lilishutumu vikosi tiifu kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Fayez al-Sarraj kuendesha shambulio hilo kwa ushirikiano na mamluki kutoka Chad. Lakini serikali ya Tripoli imeendelea kupuuzia madai hayo.

Kwenye video zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, kunaonekana vijana wenye silaha ambao wanasherehekea ushindi wao kwenye eneo hilo wakiongea kwa lugha ya Kiarabu kinachozungumzwa nchini Chad. Saa chache baadae askari kutoka miji jirani ilikuja kusaidia jeshi la ANL la Marshal Khalifa Haftar na kufaulu kurejesha kwenye himaya yake ngome hiyo iliyokuwa imedhibitiwa.

Libya inaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu, kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.