Pata taarifa kuu
NAMIBIA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wananchi wa Namibia wapiga kura kuwachagua viongozi wao

Raia wa Namibia wanapiga kura leo Jumatano katika Uchaguzi Mkuu kuwachagua viongozi wao. Namibia inaendelea kushuhudia mdororo wa uchumi na kukithiri kwa ufisadi.

Tintenpalast, Makao makuu ya Serikali na Bunge la Windhoek, mji mkuu wa Namibia.
Tintenpalast, Makao makuu ya Serikali na Bunge la Windhoek, mji mkuu wa Namibia. GNU Free Documentation License
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Namibia wameendelea kutoa malalamiko yao dhidi ya mgogoro na ufisadi ambao umekithiri kwa kiasikikubwa. Licha ya kukabiliwa na upinzani uliyotawanyika, rais anayemaliza muda wake Hage Geingob, 78, na chama chake cha Swapo wanapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo na kuendelea kusalia tena madarakani kwa kipindi cha miaka mitano.

Hata hivyo Hage Geingob, 62, anakabiliwa na upinzani mkuba kutoka kwa Panduleni Itula mmoja wa vigogo wa chama cha Swapo aliyejitenga.

Licha ya utajiri wake wa rasilimali za asili, pamoja na madini ya uranium, almasi, samaki na ukuaji wa utalii, Namibia imeshuhudia kwa miaka kadhaa mdororo wa uchumi.

Kushuka kwa bei ya bidhaa na ukame unaoendelea kwa misimu kadhaa vimeshusha mapato yake ya ndani kwa miaka miwili mfululizo (2017 an 2018) na ukosefu wa ajira kwa mwaka wa 2017 na 2018) na ukosefu wa ajira ambao unaathiri theluthi moja ya wakazi wake (34%).

Utawala wa Rais Geingob pia umekumbwa na kashfa za ufisadi.

Wiki chache zilizopita, shirika la Wikileaks lilichapisha maelfu ya nyaraka zilizoshutumu maafisa wa serikali kwa kupokea rushwa sawa na dola milioni 10 kutoka kwa kampuni ya uvuvi ya Iceland.

Mawaziri wawili walioshtakiwa katika kesi hiyo walilazimika kujiuzulu siku chache kabla ya uchaguzi, ambapo mmoja wao alizuiliwa kwa muda mfupi.

Rais wa nchi hiyo alikataa kuhusika kwake katika kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.