Pata taarifa kuu
DRC-MAZINGIRA-MAJANGA YA ASILI

DRC: Mvua kubwa yaua watu thelathini na sita Kinshasa

Watu wasiopungua 36 wamefariki dunia baada ya mvua kubwa kunyesha Jumatatu usiku wiki hii katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, Naibu Gavana wa  mji huo, Neron Mbungu amesema.

Kinshasa, DRC, Barabara kuu ya Juni 30 yakumbwa na mafuriko, Oktoba 25, 2019.
Kinshasa, DRC, Barabara kuu ya Juni 30 yakumbwa na mafuriko, Oktoba 25, 2019. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

"Waziri wa Mambo ya Ndani wa mkoa ametoa taarifa ya vifo vya watu 36. Zoezi la kutafuta miili mingine ya watu waliofariki dunia au manusura linaendelea. Uharibifu wa vifaa na hasara kwa binadamu ni kubwa, "amesema Neron Mbungu, ambaye amebaini kwamba amezuru eneo lililoathirika.

Waathiriwa walipelekwa na maporomoko ya udongo. Madaraja mawili yameporomoka na barabara inayoelekea chuo kikuu katika Wilaya ya Lemba, imeharibika vibaya, ameongeza Naibu Gavana.

"Kuna mafuriko," amebaini Neron Mbungu, huku akisema kuwa "mtoto mmoja aliyeuawa na umeme" ni miongoni mwa waathiriwa.

Barabara yakwenda chuo kikuu cha Kinshasa zimegawanyika vipande viwili kutokana na mafuriko. (26-11-2019)
Barabara yakwenda chuo kikuu cha Kinshasa zimegawanyika vipande viwili kutokana na mafuriko. (26-11-2019) Freddy Tendilonge

Mamia ya watu walfariki dunia kutokana na mmomonyoko na maporomoko mapema mwezi Januari 2018 katika mji wa Kinshasa baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha. Kinshasa mji wa tatu wenye watu wengi barani Afrika, una wakaazi milioni 10, ambao wengi wao wanaishi katika nyumba ambazo ni rahisi kuporomoka mvua inaponyesha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.