Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-AJALI

DRC: Ajali ya ndege ndogo yaua watu zaidi 29

Watu zaidi ya 29 wameuwa baada ya ndege ndogo aina ya Dornier ya shirika la ndege la Busy Bee kuanguka katika kitongoji chenye wakaazi wengi cha Birere katika mji wa Goma, mkoani Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ndege imeanguka katika kitongoji chenye wakaazi wengi cha Birere, Goma.
Ndege imeanguka katika kitongoji chenye wakaazi wengi cha Birere, Goma. AFP Photos/Pamela Tulizo
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo aina ya Dornier 228 ilikuwa ikisafiri kwenda Beni, kilomita 350 kaskazini mwa mji wa Goma, Mashariki mwa DRC, kwa mujibu afisa wa shirika hilo la ndege aliyehojiwa na RFI.

Ndege hiyo ilianguka katika kitongoji chenye wakaazi wengi cha Mapendo katika eneo la Birere linalozunguka uwanja wa ndege wa Goma dakika tatu tu baada ya kuondoka kwenye uwanja huo.

Kufikia sasa, karibu miili 29 imeondolewa chini ya vifusi vya nyumba, kwa mujibu wa meya wa mji wa Goma. Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi imetangaza kwamba watu 26 ndio wamepoteza maisha katika ajali hiyo. Idadi ya abiria walio katika ndege hiyo bado haijajulikana, lakini maafisa wa shirika la ndege la Busy Bee limesm akuwa ndege hiyo ilikjuwa imeabiri watu zaidi ya kumi na tano. Vyanzo hivyo vimebaini kwamba ajali ya ndege hiyo imetokana na tatizo la kiufundi.

Taarifa ya awali iliyotolewa na gavana wa jimbo la kivu kaskazini imesema ajali ilitokea baada ya ndege hiyo mali ya kampuni binafsu ya Busy Bee iliyokuwa safarini kwenda mji wa Beni kushindwa kuruka.

Watu saba wa familia moja ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha, Watu hao walikuwa wakiishi katika nyumba ambayo imeangukiwa na dege hiyo. Mambo Zawadi, mmoj awa viongozi wa mashirika ya kiraia mashariki mwa DRC, ni miongoni mwa abiria waliokuemo katika ndege hiyo, ambao wamefariki dunia.

Nyumba kadhaa ziliharibiwa baada ya ndege hiyo kuanguka.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umesema umetuma kikosi cha uokozi kwenda eneo la tukio pamoja na magari mawili ya kuzima moto kuzisaidia mamlaka nchini DRC.

Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini DRC kutokana na matengezo hafifu ya ndege na kiwango cha chini cha usalama kwenye usafiri wa anga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.