Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria yaendelea kukumbwa na maandamano ya usiku, watu kadhaa wakamatwa

Ikiwa imesalia wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 12, waandamanaji wameendelea kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo katika mazingira yaliyopo hivi sasa.

Mamia ya waandamanaji wamemiminika mitaani Alhamisi usiku katika maeneo mengi ya mji wa Algiers wakipinga uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 12.
Mamia ya waandamanaji wamemiminika mitaani Alhamisi usiku katika maeneo mengi ya mji wa Algiers wakipinga uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 12. © REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Katika maandamano yaliyofanyika Alhamisi jioni wiki hii katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, waandamanaji kadhaa wamekamatwa na polisi, wakati wa operesheni ya kuzima maandamano hayo.

Mamia ya watu wameingia mitaani wakipinga kufanyika kwa uchaguzi na mabadiliko ya mfumo katika uongozi wa serikali ya Algeria.

Siku ya Jumatano, watu kadhaa walikamatwa, kwa mujibu wa shirika linalotetea kuachiliwa huru kwa wafungwa.

Maandamano haya hufanyika kila Jumanne na kila Ijumaa kwa miezi kadhaa sasa.

Kwa upande wake shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty international limevishutumu vyombo vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakamata waandamanaji ambapo inadaiwa watu 29 wanashikiliwa na polisi mjini Algiers.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.