Pata taarifa kuu
SENEGAl-UFARANSA-USHIRIKIANO

Senegal na Ufaransa zakubaliana kupambana dhidi ya uhamiaji haramu

Waziri Mkuu wa Ufaransa Édouard Philippe yuko Dakar kwa ziara rasmi ya siku mbili, akiandamana na ujumbe mkubwa wa viongozi wa serikali, wabunge, viongozi wa makampuni, na wawakilishi wa ulimwengu wa utamaduni na michezo.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Édouard Philippe akizungumza na Rais wa Senegal Macky Sall kwenye Ikulu ya rais Dakar, Jumapili, Novemba 17, 2019.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Édouard Philippe akizungumza na Rais wa Senegal Macky Sall kwenye Ikulu ya rais Dakar, Jumapili, Novemba 17, 2019. © RFI/Charlotte Idrac
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inalenga zaidi usalama katika mkutano unaofunguliwa jijini Dakar Jumatatu wiki hii na ambao unaonyesha, kwa mujibu wa serikali za nchi hizi mbili, "uhusiano maalum" kati ya Senegal na Ufaransa.

Kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, semina ya kati ya serikali ni "zana muhimu". kutano huu unaofanyika Dakar unafuatia ule wa uliofanyika jijini Paris mwezi Oktoba 2017. Senegal ndio nchi pekee katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo mkutano wa aina hii unafanyika. Hii inaonyesha kwa nchi zote mbili "mfano" na "nguvu" ya ushirikiano wao.

Katika nyanja ya uchumi, Ufaransa inasalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa Senegal. Katika maswala ya ulinzi, Senegal, inayochukuliwa kama "nchi yenye usalama wa kutosha" katika ukanda huo, ambayo imeshirikishwa katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma), licha ya kuwa sio mwanachama wa G5 Sahel, ina "jukumu muhimu" kwa kusimamia amani kwa mujibu wa Paris, ambayo inasisitiza kuhusu kutolea "mafunzo" vikosi vyake vya ulinzi na usalama.

Kwa ziara hii ya Édouard Philippe, Senegal na Ufaransa zimetia saini mikataba saba, ikiwa ni pamoja na kuthibitishiwa mkopo wa sera ya umma kutoka kwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wa Euro milioni 50 kuhusu utawala wa kifedha. Na mkataba wa kupewa manuari tatu za doria kwa kikosi cha wanamaji cha Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.