rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria

Imechapishwa • Imehaririwa

Nigeria yaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya wanajihadi

media
Kambi ya Rann iliyoshambuliwa na jeshi la Nigeria Kaskazini mwa Jimbo la Borno Januari 17, 2017. Médecins sans Frontières (MSF) / AFP

Wanajeshi 10 wa Nigeria wameuawa na wengine zaidi ya 9 wamejeruhiwa katika shambulio la kushtukiza lililotekelezwa na wanajihadi wa kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo, vyanzo vya kijeshi vimethibitisha.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msafara wa wanajeshi hao ulishambuliwa katika wilaya ya Damboa kwenye jimbo la Borno ambapo pia imearifiwa kuwa wanajeshi 12 hawajapatikana.

Wapiganaji wenye uhusiano na kundi la Islamic State wamekiri kuhusika katika shambulio hilo, ambapo wamesema waliwaua wanajeshi zaidi ya 22.

Tangu kuibuka kwa makundi ya kijihadi Kaskazini mwa nchi hiyo, watu zaidi ya elfu 35 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 2 wamelazimika kukimbilia nchi jirani.

Mashambulizi haya yametekelezwa wakati huu ambapo mataifa ya magharibi yakifanya operesheni za pamoja kujaribu kuyadhibiti makundi ya kiislamu ambayo yameendelea kutatiza usalama kwenye nchi zao.