Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Polisi yawaokoa watu 259 kutoka nyumba mpya ya mateso

Polisi ya Nigeria imefanikiwa kuwaokoa watu 259 kutoka nyumba mpya ya mateso inayomilikiwa na Msikiti wa Ibadan, Kusini Magharibi mwa Nigeria ambako wamekuwa wanazuiliwa na kupata mateso.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwahutubia wakaazi wa Ibadan.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwahutubia wakaazi wa Ibadan. REUTERS/Akintunde Akinleye
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wameokolewa katika operesheni ya polisi inayoendelea nchini kote tangu wiki za hivi karibuni. Wanaume, wanawake na watoto walikua wamezuiliwa na kushikilia mateka katika kituo kisicho halali kinachomilikiwa na Msikiti wa Ibadan, Kusini Magharibi mwa Nigeria, msemaji wa polisi katika Jimbo la Oyo Fadeyi Olugbenga ameliambia shirika la Habari la AFP.

Polisi imeingilia kati "haraka" baada ya kupata habari kutoka kwa kijana wa miaka 18 ambaye alitoroka kutoka kituo hicho, Fadeyi Olugbenga amebainisha.

Kwa jumla, "watu 259 walikuwa wamefungwa na kuomba msaada wakati tulipofika," Bw Olugbenga amesema, na kuongeza kuwa watoto, vijana, watu wazima na mwanamke mmoja aliye na mtoto ni miongonu mwa watu waliookolewa.

"Baadhi wamekuwa wanazuiliwa katika kituo hicho kwa miaka kadhaa na wana tatizo za kiafya, kwa sasa wanapata huduma ya matibabu," amesema Bw Olugbenga. "Wale tuliowahoji wamesema wamekwa wanapewa chakula mara moja kwa kila siku 3, wakati mwingine mara moja au mara mbili."

Mmiliki wa nyumba hiyo na wengine wanane wamekamatwa, lakini "uchunguzi bado unaendelea ili kupata maelezo zaidi," ameongeza Bw Olugbenga.

Operesheni na mashambulizi kadhaa yaliendeshwa katika "vituo hivi vya kidini" nchini Nigeria tangu mwezi Septemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.