rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Vyombo vya Habari

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwanahabari mmoja auawa Ituri ,wawili watunukiwa tuzo ya RFI

media
Mtalaam wa Ebola nchini DRC. REUTERS/James Akena

Mtangazaji mmoja wa kituo cha redio ambaye alikuwa akijihusisha pakubwa katika kampeni ya vita dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kaskazini mwa jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameuawa akiwa nyumbani kwake, taarifa ya jeshi imethibitisha.


Kwa mujibu wa jeshi, watu waliokuwa na mapanga na visu walivamia makazi yake kwenye mtaa wa Lewebma ambapo walimuua kwa kumchoma visu
kisha kumjeruhi mke wake na kuchoma moto nyumba yao.

Mhariri wa Redio Lwemba, amesema mwenzao Papy Mumbere, aliuawa wakati akirejea nyumbani  kwake kutoka studio ambako alikuwa amefanya kipindi maalumu kuhusu Ebola.

Mkuu wa wilaya ya Mambasa Franklin Yakani, amesema wapiganaji wa kundi la Mayi-Mayi ndio wahusika wa mauaji ya mwandishi huyo wa habari.

Wakati huo huo waandishi wawili wa habari kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wametunukiwa tuzo ya RFI inayotolewa kwa heshima ya kuwaenzi wanahabari wake wawili Ghislaine Dupont na Claude Verlon ambao waliuawa miaka 6 iliyopita kwenye mji wa Kidal, Kaskazini mwa nchi ya Mali.