rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Zoezi la kutafuta miili ya watu Bafoussam laanza tena

media
Eneo lililokumbwa na maporomoko ya udongo ambayo yameuwa watu 43 Bafoussam Oktoba 30, 2019. REUTERS/Stringer NO RESALES. NO ARCHIVES

Zoezi la kutafuta miili ya watu iyokwama chini ya vifusi vya nyumba limeanza tena katika eneo lililokumbwa na maporomoko ya udongo katika mji wa Bafoussam mapema wiki hii.


Zoezi hilo lilisitishwa Alhamisi asubuhi, na kurudi tena kuanza jioni.

Tukio hilo la maoromoko ya udongo lililotokea JUmatatu iki hii liliuwa watu 43 na wengine 11 kujeruhiwa.

Timu ya wafanyakazi wa huduma za uokoaji wamekuwa wakipekua vifusi vya nyumba za manusura baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa kuua watu wasiopungua 43.

Polisi pia wamekuwa wakiwasaka makumi ya watu wengine walioripotiwa kutoweka katika mji wa Bafoussam katika miinuko ya magharibi umbali wa kilomita 200 kaskazini mwa mji wa bandari kuu wa Doaula. Awa Fonka Augustine Gavana wa mkoa wa Magharibi nchini Cameroon amesema kuwa ni wazi kuwa, wakazi wa eneo hilo wanapasa kuondoka katika makazi yao kwa kuzingatia kuweko uwezekano wa kujiri maafa zaidi.

Mvua kubwa zimeendelea kunyesha nchini Cameroon na hivyo kusababisha mafuriko yaliyowafanya watu karibu elfu 30 kukosa makazi.

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) wiki iliyopita liliripoti kuwa, mvua zisizo za kawaida zilizoikumba Sudan Kusini pia zimebomoa vituo vya afya na barabara na kufanya huduma za chakula na maji kwa watu karibu milioni moja kuwa ngumu zaidi.