Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Kundi la UPC laongeza ushawishi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Machafuko yanaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, licha ya mkataba wa amani kulitiliwa saini hivi karibuni kati ya makundi 14 yenye silaha na serikali.

Jenerali Ali Darass katika ngome yake ya Bambari nchini Jamhuri ya Afrika Kati.
Jenerali Ali Darass katika ngome yake ya Bambari nchini Jamhuri ya Afrika Kati. © RFI/MG
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca)imelaani mwenendo wa kundi la UPC kwa kukiuka kanuni za mkataba wa amani ambao ilitia saini.

Hata kama idadi imeshuka kwa kiwango kikubwa, Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) imeorodhesha visa kati ya 50 na 70 vya ukiukaji wa mkataba wa amani kila wiki. Machafuko hayo yanahusisha makundi mawili, MLCJ na FPRC, ambayo yalitokea katika mkoa wa Birao Kaskazini mashariki mwa nchi, ambapo watu takriban 24,000 walilazimika kuyatoroka makaazi yao.

Hivi karibuni kikosi cha Umoja wa Mataifa (Minusca) kilifanya operesheni dhidi ya kundi la 3R katika eneo la Karoui, Kaskazini magharibi mwa nchi.

Wakati huo huo kundi jingine la UPC limeendelea kutuma wapiganaji wake Kusini Mashariki mwa nchi.

Raia wameendelea kuwa na wasiwasi katika maneo mbalimbali ya nchi hiyo licha ya makundi hayo na serikali kutia saini kwenye mkataba wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.