Pata taarifa kuu
URUSI-AFRIKA-SIASA-UCHUMI

Nini kilikubaliwa katika mkutano kati ya Urusi na viongozi wa Afrika ?

Rais wa Urusi Vladimir Putin, wiki hii, aliongoza mkutano wa kwanza kati ya Urusi na Afrika, siku ya Jumatano na Alhamisi, katika mji wa pwani wa Sochi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na viongozi wa Afrika katika mkutano wa Afrika na Urusi, mjini Sochi 24/10/2019
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na viongozi wa Afrika katika mkutano wa Afrika na Urusi, mjini Sochi 24/10/2019 Sergei Chirikov/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, ulilenga kuisaidia Urusi kuimarisha ushawishi wake barani Afrika katika masuala ya usalama na biashara.

Rais Putin ameahidi kuongeza mara mbili kiwango cha uwekezaji barani Afrika baada ya kuafikiana kuhusu masuala mbalimbali:

Masuala ya kijeshi na siasa:

-Urusi imetia saini mkataba na serikali ya Nigeria, ili kuuziwa Helikopta 12 aina ya Mi-35 Hind E.

-Aidha, Urusi inapanga kuuza silaha zenye thamani ya Dola Bilioni 4 katika nchi mbalimbali barani Afrika mwaka 2019.

-Putin pia amesema tayari Urusi, imesamehe deni la Dola Bilioni 20 kwa mataifa mbalimbali barani Afrika.

-Urusi pia imeahidi kusaidia kumaliza mizozo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan.

Nishati:

-Kampuni ya serikali ya Urusi kujenga vinu vya Nyuklia kwa lengo la kuzalisha umeme nchini Ethiopia.

-Benki ya kitaifa nchini Urusi, kituo cha uwekezaji nchini humo imetia saini mkataba na serikali ya Congo Brazaville kujenga bomba la mafuta.

-Aidha, imetia saini makubaliano na serikali ya Morocco kuisaidia katika kusafisha mafuta ghafi.

Uchumi na biashara:

-Benki kubwa inayotoa mkopo Sberbank, VEB na kituo cha usafirishaji kimeshirikiana na kituo cha uwezekaji jijini London Gemcorp, kitatoa Dola Bilioni 5 kusaidia uwekezaji katika mataifa ya Afrika.

-Mkataba huo utasaidia kutoa msaada wa fedha katika nchi ya Angola, Ethiopia, Msumbiji na Zimbabwe.

Mipango ijayo kati ya Urusi-Afrika:

-Uwekezaji kati ya Urusi na Afrika imeongezeka mara mbili kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na kufikia zaidi ya Dola Bilioni 20.

-Kiwango cha biashara kuongezeka mara mbili kwa kipindi cha miaka minne na mitano ijayo.

Uchambuzi:

Urusi bado ipo nyuma katika utoaji wa misaada na uwekezaji barani Afrika, nyuma ya Umoja wa Ulaya inayotoa Dola Bilioni 334 kila mwaka kwa ajili ya masuala ya biashara, huku China ikitoa Dola Bilioni 204.

Mtalaam wa masuala ya Urusi Samuel Ramani kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, anasema Urusi inataka kushawishi zaidi barani Afrika na kuuza bidhaa zake katika mataufa mbalimbali barani Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.