rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Wafungwa wagoma wakilalamikia ukosefu wa huduma ya afya Bukavu

media
Makao makuu ya manispaa ya jiji la Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini, DRC. Wikimedia

Wafungwa 45 wamefariki dunia katika gereza kuu la Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwanzo wa mwaka huu kwa kukosa huduma ya afya.


Gereza hilo lenye uwezo wa kupokea wafungwa kati ya 350 na 500 lililojengwa tangu enzi za ukoloni, lakini kwa sasa lina karibu wafungwa elfu mbili.

Wafanyakazi wa afya wanaofanya kazi katika gereza hilo, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamethibitisha taarifa hiyo.

“Wafungwa 45 wamepoteza maisha, tangu Januari mwaka huu kwa sababu ya ukosefu wa huduma ya afya”, mmoja wa wafanyakazi hao ambao hakutaja jina aliyenukuliwa na mwandishi wetu mjini Bukavu, William Basimike, amebaini.

Wengine walihamishwa katika Hospitali kuu ya mjini Beni, lakini hakukuwa na dawa na vifaa vya kuwasaidia kupata huduma hiyo.

Hali hii imesababisha wafungwa kugoma wakilalamikia ukosefu wa dawa na vifaa vya kufanya vipimo.