Pata taarifa kuu
CAMEROON-HAKI-SIASA

Wafuasi 22 wa chama cha upinzani Cameroon waachiliwa huru

Wafusi 22 wa chama cha upinzani cha MRC nchini Cameroon, wameachiliwa huru kwa dhamana lakini watarejea Mahakamani tarehe 7 mwezi Desemba.

Rais wa Cameroon Paul Biya, Desemba 31, 2018.
Rais wa Cameroon Paul Biya, Desemba 31, 2018. RFI/Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Walikamatwa mwaka 2018, baada ya kushiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku, kupinga kuchaguliwa kwa rais Paul Biya wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Kiongozi wa chama hicho Maurico Kamto, ambaye ameendelea kusema kuwa rais Biya aliiba Uchaguzi, naye aliachuliwa huru baada ya kuwa jela miezi tisa.

Rais Paul Biya ametaka mashtaka dhidi ya wapinzani wake kuondolewa.

Hivi karibuni Rais wa Cameroon Paul Biya aliamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa 333 wanaoshtumiwa kuhusika katika mgogoro uliozuka katika maeneo yanayozungumza Kiingereza. Hatua ambayo ilichukuliwa wakati "mazungumzo ya kitaifa" yalikuwa yakiendelea.

Rais Paul Biya alitangaza hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo mmoja wa viongozi wa wanaharakati wanaotaka maeneo yao kuwa taifa huru, Julius Ayuk Tabe, aliyejitangaza rais wa Ambazonia, ambaye anatumikia kifungo cha maisha jela tangu miezi michache iliyopita katika jela kuu la Yaoundé, anaendelea kusalia jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.