Pata taarifa kuu
UNICEF-WATOTO-HAKI

UNICEF: Mmoja kati ya watoto watatu anakabiliwa na utapia mlo au kupoteza uzito

Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa leo Jumanne ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto duniani UNICEF, Theluthi moja ya watoto chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na utapia mlo, huku shirika hilo likisisitiza kuhusu utapia mlo kuwa na sura nyingi katika karne hii ya 21.

Unga huu wa spirulina, pia ni nyongeza ya chakula ambao hutumika kupambana na utapiamlo duniani.
Unga huu wa spirulina, pia ni nyongeza ya chakula ambao hutumika kupambana na utapiamlo duniani. Music4thekids/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

UNICEF imesema utapia mlo kwa miaka 20 iliyopita umechukua sura kadhaa: ni kati ya utapiamlo, ambao unaweza kubadilisha ukuaji wa mwili na utambuzi wa watoto kuwa wazito.

Sura ya kwanza, ambayo imekuwa ikijulikana kila wakati, inahusiana na njaa. Ukosefu wa Chakula bado unaendelea kuwa shida kwa mamilioni ya watoto duniani, ingawa hali hiyo imeboreka kwa sasa ulimwenguni, amesema Noël Marie Zagré, mshauri wa lishe katika shirika la UNICEF barani Afrika.

Ulimwenguni kote, theluthi mbili ya watoto hawana chakula cha kutosha. Karibu nusu ya wale wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 2, hawapati matunda na mbogamboga, Noël Marie Zagré ameongeza.

Mwaka 2016 utafiti mpya ulieonya juu ya ongezeko la uzito mkubwa wa watu duniani ambao unaweza kusababisa kusambaa kwa kasi kwa utapia mlo.

Kwa kawaida,utapia mlo unaweza kuhusishwa na njaa. Lakini katika ripoti hiyo ya utapiamlo kimataifa ya mwaka 2016, ilionesha kuwa watu walio na uzito mkubwa umeathiri mamilioni ya watu pia na kusababisha utapia mlo.

Watu hao utafiti, ulibaini kuwa wanatumia sukari kwa kiwango kikubwa,chumvi au mafuta katika damu zao na hawapati lishe bora.

Ripoti hiyo ilionya pia juu ya suala la afya kwa ujumla na maendeleo, na kutaka rasilimali zaidi kuwekezwa ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaweza kuleta athari kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.