Washington yaweka vikwazo dhidi ya familia ya Gupta
Marekani imeweka vikwazo dhidi ya familia tajiri ya Gupta, inayohusishwa kwa kashfa ya ufisadi nchini Afrika Kusini, Wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza katika taarifa Alhamisi wiki hii.
Imechapishwa:
Ajay, Atul na Rajesh Gupta, wanaoshtumiwa kuhusika "katika kashfa kubwa ya ufisadi na hongo ili kupata mikataba ya serikali" wamewekwa kwenye orodha nyeusi ya vikwazo.
Familia ya Gupta, ambayo ilikuwa na uhusiano wa karibu na rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, inatuhumiwa "kuiba mamia ya mamilioni ya dola kupitia miradi haramu na serikali," Wizara ya Fedha ya Marekani imeaongeza.
Familia hiyo ya Gupta imekuwa kwenye shutuma za muda mrefu kuhusu kutumia urafiki wao na rais Jacob Zuma kujinufaisha kisiasa kwaajili ya manufaa ya biashara zao.