rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tunisia

Imechapishwa • Imehaririwa

Mgombea urais anayezuiliwa jela aomba uchaguzi kuahirishwa Tunisia

media
Mfanyabiashara na mmiliki wa kituo cha televisheni Nessma, Nabil Karoui, Agosti 2, 2019. © REUTERS/Zoubeir Souissi/File Photo

Wakati wananchi wa Tunisia wanaendelea kusubiri kutangazwa kwa matokeo kamili na rasmi ya uchaguzi wa wabunge, mgombea urais Nabil Karoui, aliyechukuwa nafasi ya pili katika duru ya kwanza ya uchaguzi, anataka duru ya pili ya uchaguzi huo kusogezwa mbele.


Matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumapili Oktoba 5 yanatarajiwa kutangazwa leo Jumatano Oktoba 9.

Duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge imepangwa kufanyika Jumapili Oktoba 13.

Wagombea wawili Kais Saied na Nabil Karoui wanatarajia kupambana katika uchaguzi huo, baada ya kupata kura zinazowaruhusu kushiriki duru ya pili ya uchaguzi.

Mawakili wa Bw Karoui wamewasilisha malalamiko yao Jumanne asubuhi wiki hii kwenye Mahakama ya Kiutawala ya Tunis. Habari hii imethibitishwa na Abdelaziz Belkhodja, msemaji wa Nabil Karoui.

Abdelaziz Belkhodja amedai ukiukaji wa usawa wa fursa wakati mteja wake, ambaye ni mgombea urais, anaendelea kuzuiliwa jela tangu Agosti 23 mwaka huu.