Pata taarifa kuu
TUNISIA-UCHAGUZI-SIASA

Wagombea binafsi wapata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge Tunisia

Wapiga kura nchini Tunisia hawakujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa wabunge wa tarehe 7 Oktoba nchini humo, huku wagombwa wengi binafsi wakipata kura na hivyo kuwaruhusu kushiriki katika Binge la nchi hiyo.

Wabunge wa Tunisia wakati wa kikao cha bunge Aprili 25, 2017.
Wabunge wa Tunisia wakati wa kikao cha bunge Aprili 25, 2017. FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa itakuwa ngumu kwa muundo wa serikali mpya.

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa wabunge wa Tunisia yatatangazwa Jumatano Oktoba 9. Uchaguzi huo ulishuhudia kiwango cha chini cha ushiriki ambacho kilifikia asilimia 41.

Tunisia inakabiliwa na mvutano wa kisiasa baada ya uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa wiki iliyopta.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa, hakuna chama kilichopata ushindi unaohitajika ili kuunda serikali.

Licha ya chama cha Kiislamu cha Ennahda kuonekana kuwa mbele, itabidi chama hicho kipate uungwaji mkono wa vyama vingine, ili kuunda serikali.

Yamina Zoglami, afisa wa juu wa chama cha Ennahda amesema, chama hicho kitakuwa na kibarua ya kuunda serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.