rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tunisia

Imechapishwa • Imehaririwa

Tunisia: Vyama viwili hasimu vyaadai kuongoza katika uchaguzi wa wabunge

media
Mmoja kati ya wapiga kura akiweka kura yake katika sanduku la kupigia kura Tunis, wakati wa uchaguzi wa wabunge Oktoba 6, 2019. © REUTERS/Zoubeir Souissi

Vyama viwili hasimu ncini Tunisia, Ennahdha kile cha na mgombea urais anazuiliwa Nabil Karoui, vyote vinadai kuongoza katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika jana Jumapili nchini humo.


Uchunguzi uliochapishwa na taasisi tofauti nchini Tunisia hata hivyo umebaini kwamba chama cha Ennahdha chenye itikadi za Kiislam kimeshinda idadi kubwa ya viti, 40 kati ya 217, dhidi ya 33 hadi 35 kwa chama cha Bwana Karoui.

Vyama hivi viwili, ambavyo vimedai ushindi mbele ya waandishi wa habari bila kutoa takwimu, vilifutilia mbali muungano wowote wakati wa kampeni.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumatano wiki hii, mamlaka inayosimamia uchaguzi (ISIE) imebaini.

Ikiwa uchunguzi huu utathibitishwa, chama cha Ennahdha kitakuwa kimepoteza tena idadi ya viti na Bunge jipya linaonekana kugawanyika kati ya vyama vyenye nguvu na vile vyenye wafuasi wadogo.

Hata kama kutapatikana mshindi, itakuwa ngumu kwa mshindi huyu kukusanya idadi kubwa ya viti, tofauti na mwaka 2014, wakati Bunge liligawanywa kati ya chama cha Nidda Tounes, na Ennahdha, ambavyo vilishikilia idadi kubwa ya viti na mara moja viliamua kuungana.