Pata taarifa kuu
CAMEROON-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mgogoro Cameroon: Paul Biya aamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa 333

Rais wa Cameroon Paul Biya ameamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa 333 wanaoshtumiwa kuhusika katika mgogoro uliozuka katika maeneo yanayozungumza Kiingereza. Hatua ambayo inachukuliwa wakati "mazungumzo ya kitaifa" yakiendelea.

Watu waliokamatwa baada ya kuzuka machafuko katika maeneo yanayozungumza Kinngereza Cameroon wakifikishwa katika mahakama ya Kijeshi ya Yaounde, Desemba 2018. (picha ya kumbukumbu)
Watu waliokamatwa baada ya kuzuka machafuko katika maeneo yanayozungumza Kinngereza Cameroon wakifikishwa katika mahakama ya Kijeshi ya Yaounde, Desemba 2018. (picha ya kumbukumbu) © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Paul Biya alitangaza hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter. "Leo nimeamua kusitisha katika mahakama ya kijeshi kesi dhidi ya watu 333 waliokamatwa na kuwekwa kizuizini kwa makosa yaliyofanywa baada ya kuzuka machafuko katika mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa nchi. "

Kwa hivyo, hatua hii haiwahusu watu ambao tayari wamehukumiwa kufuatia kuzuka kwa machafuko hayo, kama mmoja wa viongozi wa wanaharakati wanaotaka maeneo yao kuwa taifa huru, Julius Ayuk Tabe, aliyejitangaza rais wa Ambazonia, ambaye anatumikia kifungo cha maisha jela tangu miezi michache iliyopita katika jela kuu la Yaoundé.

Uamuzi huu uliwasilishwa mara moja Alhamisi alaasiri na Waziri Mkuu katika makao makuu ya Bunge , ambapo "mazungumzo ya kitaifa" kuhusu mgogoro katika maeneo yanayozungumza Kiingereza yanaendelea. Ni "hatua ya nia njema" ambayo Rais Paul Biya "amechukuwa wakati tunaendelea na shughuli zetu," amesema Joseph Dion Ngute.

Rais wa Jamhuri, kulingana na hadhi anayopewa na Katiba, anayo haki ya kusimamisha kesi ikiwa anaona kuwa kusitishwa kwa kesi hiyo kuna faida kubwa upande wa Serikali. Na ndivyo alivyofanya rais ili kuonyesha nia yake njema, Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute amesema,.

Hatua hiyo imeshangiliwa na umat wa watu waliokuwa wakishiriki katika mazungumzo hayo ya kitaifa, hata kama watu wanaohusika na hatua hiyo hawajatambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.