Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA-HAKI

Wafuasi wa Karoui kukabiliana na uchaguzi ikiwa mmoja wa wagombea atasalia jela

Kampeni za uchaguzi nchini Tunisia zinafungua leo Alhamisi kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Uchaguzi huo, ambao umepangwa kufanyika Oktoba 13, utawakutanisha Kais Saied na mfanyabiashara alinayezuliwa jela Nabil Karoui.

Magazeti mbalimbali yachapisha picha wagombea wawili katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Tunisia, Septemba 18, 2019.
Magazeti mbalimbali yachapisha picha wagombea wawili katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Tunisia, Septemba 18, 2019. © REUTERS / Zoubeir Souiss
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Bw Karoui wamesema kuwa hawatakubali kufanyika kwa uchaguzi huo ikiwa mmoja wa wagombea hao wawili atakuwa bado anazuiliwa jela.

Kufungwa kwa Nabil Karoui kumezua sintofahamu kwa uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki ijayo. Wajumbe kadhaa wa kamati kuu ya kisiasa ya chama chake cha Qalb Tounes walikutana Jumatano (Oktoba 2). Wametilia mashaka duru ya pili ya uchaguzi wa urais ikiwa kiongozi wao atakuwa bado anazuiliwa jela ndani ya siku 11 zinazosalia.

Wameomba Tume huru ya uchaguzi, ISIE kutafuta suluhisho haraka. "Ni juu yao leo kutafutia suluhu hali ambayo sio ya kawaida inayomkabili mgombea wetu aliyechaguliwa akiwa jela. Wanapaswa kupata ufumbuzi, sio sisi, " Osama Khlifi, mjumbe wa kamati kuu ya kisiasa ya chama cha Qalb Tounes amesema.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi, ISIE, ameomba mara kadhaa Nabil Karoui kuachiliwa huru ili kuhakikisha usawa kuwania na fursa kwa wagombea wote wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.