Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Maswali yaibuka baada ya mashambulio ya Boulkessi, Mali

Eneo la katikati mwa Mali lilikumbwa na mashambulizi mawili usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, yaliyosababisha vifo kadhaa vya askari wa nchi hiyo.

Askari wa Kikosi cha wanajeshi wa Mali (Fama) katika kituo cha jeshi cha Anderamboukane katika mkoa wa Menaka nchini Mali, Machi 22, 2019.
Askari wa Kikosi cha wanajeshi wa Mali (Fama) katika kituo cha jeshi cha Anderamboukane katika mkoa wa Menaka nchini Mali, Machi 22, 2019. Agnes COUDURIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia wawili waliuawa katika mji wa Mondoro. Na katika mji mwingine wa Boulkessi, askari 25 waliuawa na askari 70 katika shambulio dhidi ya kambi ya kikosi cha pamoja cha G5 Sahel kutoka Mali, huku askari wengi 70 hawajulikani waliko mpaka sasa.

Saa chache tu baada ya mashambulizi hayo mawili, jeshi la pamoja la G5 Sahel lilinyooshea kidolea cha lawama Ansarul Islam, kundi la kigaidi kutoka nchini Burkina Faso. Kwa mujibu wa taarifa, kundi la Ansarul Islam ndilo lilishambulia kambi za jeshi la Mali katika miji ya Mondoro na Boulkessi.

Sio shambulio la kwanza kutokea katika mji wa Boulkessi, mji unaopatikana kwenye mpaka na Burkina Faso. Machi 15, mkuu wa kijiji alitekwa nyara na "watu wenye silaha kutoka nchi jirani," kulingana na mkuu wa mkoa wakati huo wa kisa hicho cha kutekwa nyara. "Hili ni eneo la Jafar Dicko, kiongozi wa kundi la Ansarul Islam. Anahubiri mara kwa mara katika eneo hili, "amesema mkaazi mmoja wa Bulkessi.

Pia katika kijiji hiki, mnamo mwaka 2017 wakati kundi la wanamgambo wa KIislamu la GSIM lilipoanza harakati zake, lilikiri kuendesha sahambulio lake la kwanza dhidi ya jeshi la Mali (FAMA).

Katika eneo hili la mpakani, pia kunaripotiwa kundi la Islamic State katika ukanda wa Sahara. Kulingana na taarifa kutoka idara ya ujasusi ya Burkina Faso, kundi la EIGS, tawi la Abdulakim, lilipanga na kutekeleza shambulio Agosti 19 katika mji wa Koutougou ambapo askari 24 wa Burkina Faso walipoteza maisha. Pia kulingana na taarifa hiyo, baada ya shambulio hilo, washambuliaji walitawanyika. Wengine waliingia katika mji wa Boulkessi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.