Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIASA-HAKI

Rais wa Liberia afutilia mbali wito wa uundwaji wa Mahakama maalum kuchunguza mauaji

Rais wa Liberia George Weah amekataa wito na shinikizo za Kimataifa, kuunda Mahakama maalum kuchunguza mauaji ya zaidi ya watu 250,000 wakati wa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rais wa Liberia George Weah.
Rais wa Liberia George Weah. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Rais Weah amebainisha hilo, baada ya kurejea nyumbani akitokea kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Weah amesema haelewi, wanaharakati wanachokitaka, kwa sababu tangu alipoingia madarakani, hajawahi kusema kuwa ataunda Mahakama hiyo.

Akishangiliwa na wafuasi wake, mchezaji huyo wa zamani wa mchezo wa soka amesema kuwa kazi kubwa aliyonayo ni kuinua uchumi wa taifa hilo miongoni mwa masuala mengine muhimu.

Msimamo wa rais Weah, umewasikitisha wanaharakati wa haki za binadamu ambao walikuwa na matumaini makubwa kuwa angeamuru kuundwa kwa Mahakama hiyo.

Rais Weah ni rais wa pili kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya nchi hiyo,baada ya kumalizika kwa vita vya muda mrefu kati ya mwaka 1989 hadi 1997.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.