Pata taarifa kuu
CAMEROON-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mazungumzo makubwa ya kitaifa kuanza Jumatatu hii Cameroon

Mazungumzo makubwa ya kitaifa yatakayoleta pamoja wadau wote katika mzozo wa Cameroon, yanaanza leo Jumatatu Septemba 30 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Yaounde.

Mazungumzo makubwa ya kitaifa "yaliyoitishwa na Rais Paul Biya , wengi  wana matumaini kuwa yatazaa matunda.
Mazungumzo makubwa ya kitaifa "yaliyoitishwa na Rais Paul Biya , wengi wana matumaini kuwa yatazaa matunda. © REUTERS/Carlo Allegri -/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya washiriki wanatarajiwa kupata suluhu ya kuondokana na mzozo unaoyakumba maeneo yanayozungumza Kiingereza, mzozo ambao tayari umesababisha vifo vya watu 3,000 katika kipindi cha miaka 3, huku watu karibu nusu milioni wametoroka makaazi yao na wakimbizi 40,000 wamepewa hifadhi ya ukimbizi katika nchi jirani. Mazungumzo haya makubwa "ya kitaifa" yaliyoitishwa na Rais Paul Biya yanatarajia kuleta matumaini mengi nchini Cameroon, lakini pia wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia.

Wengi wanaona kwamba mazungumzo haya yatazaa matunda kutokana na utashi wa rais mwenyewe kuitisha mazungumzo hayo. Jambo lingine la tumaini ni kuona wadau mbalimbali wamekubali kushiriki mazungumzna hayo, huku jumuiya ya kimataifa ikionekana kutilia mkazo mazungumzo hayo.

Hata hivyo kuna baadhi ya waangalizi ambao wanaona kuwa mazungumzo hayo hayana umuhimu wowote kutokana na kukosekana kwa mpatanishi asiegemea upande wowote kwa sababu serikali ya Cameroon ni sehemu ya pande zinazohusika katika mzozo huo, kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi muhimu kutoka mashirika ya kiraia wenye ushawishi mkubwa nchini Cameroon, kutokuepo katika mazungumzo hayo kiongozi wa upinzani Maurice Kamto, ambaye anaendelea kuzuiliwa, na haswa kukosekana kwa viongozi wakuu wanaotaka maeneo yanayozumnguza Kiingereza kuwa taifa huru. Waangalizi hao wanabaini kwamba mazungumzo hayo hayajatimiza masharti.

"Tunatarajia wageni wote kushiriki mazungumzo haya ..., "amesema Gregory Owona, Naibu Katibu Mkuu wa chama tawala cha RDPC, na Waziri wa Kazi na Usalama wa Jamii.

Je! Haingekuwa bora kwanza kuweka misingi ya makubaliano ya moja kwa moja kati ya pande zinazohasimiana kabla ya kuitisha mazungumzo hayo makubwa," mmoja wa wataalam wa timu ya usuluhishi amejihoji.

"Siku 5 sio nyingi," mmoja wa washiriki amesema. "Wakati mwingine tuna maoni kwamba utawala unajaribu tu kufanya zoezi la mawasiliano. Lakini mchakato huu ni ngumu sana na mustakabali wa nchi uko hatarini, " ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.