Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab washambulia kambi ya jeshi la Marekani

Wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shaba wameendesha mashambulizi mawili dhidi ya mali ya vikosi vya kigeni nchini Somalia. Katika mji wa Mogadishu, bomu limelenga msafara wa jeshi la Italia. Wakati huo huo, magaidi hao wameshambulia kambi ya jeshi la Marekani kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Mogadishu.

Msafara wa magari ya jeshi la Italia kutoka ujumbe wa mafunzo ya Umoja wa Ulaya nchini Somalia (EUTM-S) ulishambuliwa Jumatatu tarehe 30 Septemba, 2019 Mogadishu.
Msafara wa magari ya jeshi la Italia kutoka ujumbe wa mafunzo ya Umoja wa Ulaya nchini Somalia (EUTM-S) ulishambuliwa Jumatatu tarehe 30 Septemba, 2019 Mogadishu. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Hili ni shambulio ambalo wanamgambo wa Kiislamu wamefanya dhidi ya uwanja wa ndege wa Balidogle ambako kunapatikana kambi maalumu ya jeshi la Marekani, inayotumiwa na Washington kwa kufanya mashambulio ya ndege zisizo kuwa na rubani na kutoa mafunzo kwa vikosi maalum vya Somalia. Magaidi hao walifanya mashambulizi kwa kutumia magari mawili yaliyokuwa yamejaa mabomu dhidi ya jengo hilo.

Wakati huo huo kulifuata urushianaji risasi. Operesheni hiyo ilibadilishwa kuwa vita ya mawasiliano.

Katika taarifa ya kwanza, wanamgambo wa Al Shabab wamedai "wameingia katika eneo kunakopatikana kambi ya jeshi la Marekani kabla ya kutekeleza shambulio dhidi ya majengo mbalimbali katika eneo hilo." Baadaye kwenye Radio Andalus, moja ya vyombo vyake vya habari vya propaganda, wanamgambo wa Al Shaba wamedai kuwa waliwauwa askari zaidi ya mia moja na kisha kuharibu ndege tano zisizo kuwa na rubani pamoja na helikopta.

Habari hii imekanushwa mara moja na mamlaka nchini Somalia. Kwa mujibu wa wanajeshi na serikali, wanamgambo wa Al Shaba hawakuweza kamwe kuingia katika kambi ya jeshi la Marekani na wote waliuawa nje ya kambi hiyo. Hakukuwa na majeruhi katika kambi hiyo. Baadaye, Washington ililaani shambulio hilo na kupongeza jeshi la Somalia kwa kukomesha shambulio hilo bila kupoteza askari hata mmoja.

Mapigano dhidi ya Al Shamba hutokea mara kwa mara katika eneo hilo, ambalo kwa sehemu moja wanatawala. Misafara ya kijeshi wakati mwingine hulengwa kwenye barabara inayotokea Balidogle kwenda Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.